ABNA: Watu kadhaa wamekamatwa mjini Paris, Ufaransa, wakishukiwa kupanga shambulizi la kigaidi dhidi ya vikosi vya usalama. Taarifa hizo zimeripotiwa leo na gazeti la Ufaransa la Le Figaro, likinukuu waendesha mashataka wa mjini Paris. Gazeti hilo limesema washukiwa hao walipanga shambulizi baya ambalo liliwahi kuzuiwa. Washukiwa wanne bado wanashikiliwa kwa uchunguzi zaidi, ikiwa ni pamoja na kijana wa miaka 17 ambaye anajulikana na polisi. Washukiwa hao walikamatwa Ijumaa iliyopita kama sehemu ya uchunguzi kuhusu njama za kigaidi uliofunguliwa Febuari Mosi, ambao unashughulikiwa na Kurugenzi Kuu ya Usalama wa Ndani. Mashambulizi kadhaa ya kigaidi yameshuhudiwa nchini Ufaransa tangu mwkaa 2015, na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 250.
Mwisho wa habari/ 291